MOSCOW:Condoleeza Rice amekutana na wanaharakati wa haki za binadamu
13 Oktoba 2007Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleeza Rice amekutana na wanaharakati wa kutetea haki za binadamu nchini Urusi akiwa ziarani nchini humo.
Mazungumzo ya ngazi za juu yaliyojadili mpango wa Marekani wa kuweka mitambo ya kukinga makombora katika Ulaya ya Mashariki hayakufikia makubaliano.
Kufuatia mvutano uliojitokeza katika mzungumzo yaliyohudhuriwa na rais Vladimir Puttin mawaziri wa mambo ya nje wa Urusi na Marekani na wenzao wa ulinzi leo hii bibi Rice alikutana na wawakilishi wa mashirika yasiyo ya kiserikali na waziri wa ulinzi wa Marekani Robert Gates amekutana na wanfunzi wa kijeshi katika chuo cha jijeshi cha Urusi.
Baadae leo bibi Rice anatarajiwa kukutana na waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov katika dhifa ya chakula cha jioni.
Licha ya kutofikia makubaliano yoyote katika mazungumzo ya mpango wa mitambo ya kukinga Makombora katika nchi za Poland na Jamuhuri ya Czech, bibi Condoleeza Rice amesema kwamba Marekani itaendelea mbele na mpango wake.