Moscow.Mradi wa kiwanda cha Nyuklia Bushehr kuanza kazi September mwakani.
26 Septemba 2006Mradi wa kiwanda cha kuzalisha nyuklia wa Iran katika mji wa Bushehr utaanza kufanya kazi mwezi September mwaka ujao.
Afisa wa ngazi za juu wa masuala ya nyuklia nchini Urusi amesema Urusi na Iran zimesaini mkataba wa kuiruhusu Urusi kujenga mtambo wa nyuklia nchini Iran.
Taarifa hiyo imekuja wakati maafisa wa ngazi za juu wa masuala ya kinyuklia wa nchini Iran wapo nchini Urusi kwa ajili ya mazungumzo na maafisa wa Urusi yenye nia ya kuendeleza jitihada za kimataifa za kuitaka Tehran isimamishe mradi wake wa kuzalisha maadini ya Uranium.
Marekani na nchi kadhaa za magharibi zinashughulishwa na harakati za Urusi za kumaliza kujenga mradi wake huo wa nyuklia huko Bushehr uliogharimu dola milioni mia nane.
Washington ina wasi wasi kuwa kiwanda hicho kinaweza kutumiwa na Iran kuzalisha nishati kwa ajili ya silaha.