1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Moshi watanda anga ya mji wa Khartoum

29 Aprili 2023

Sauti za mashambulizi ya anga, silaha za kukabiliana na ndege za kivita na mizinga viimesikika Khartoum mapema ya leo

Sudan Karthoum | Unruhen: Brand am Flughafen
Picha: Str/REUTERS

Sauti za mashambulizi ya anga, silaha za kukabiliana na ndege za kivita na mizinga viimesikika Khartoum mapema ya leo na moshi mweusi uliotanda juu ya sehemu za jiji hilo, wakati huu ambao mapigano ya Sudan yakiingia wiki ya tatu.Mapigano kati ya jeshi na kikosi pinzani cha jeshi hilo yanaendelea licha ya tangazo la kusitisha mapigano kwa masaa 72 baada ya mashambulizi ya anga, makombora kuugubika mji wa Khartoum na mingine ya karibu ya Bahri na Ombdurman.Kutokana na mapigano hayo kwa mujibu wa rekodi za Umoja wa Mataifa takriban watu 512 wameuawa na wengine karibu 4,200 wamejeruhiwa. Hata hivyo umoja huo unaamini kuwa idadi  halisi ni kubwa kuliko hiyo iliyoainishwa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW