Mostovoy wa Urusi nje ya kikosi baada ya kuambukizwa Corona
11 Juni 2021Winga wa timu ya taifa ya Urusi Andrei Mostovoy ameondolewa katika kikosi kitakachoshiriki michuano ya mataifa ya Ulaya Euro 2020 baada ya kuambukizwa Covid-19. Soma zaidi Michuano ya mataifa ya Ulaya Euro 2020 kung'oa nanga Juni 11 hadi Julai 11
Mostovoy ni mchezaji wa kwanza kuondolewa katika kikosi cha timu zitakazoshiriki mashindano hayo baada ya kupatikana na Corona.
Kupitia ukurasa wa twitter timu hiyo imeandika kuwa nafasi ya Mostovoy itachukuliwa na beki Roman Evgeniev kutokana na hali isiyoridhisha ya majibu ya kipimo cha corona cha PCR.
Siku ya Jumamosi Urusi ina miadi na Ubelgiji katika mechi yake ya kwanza ya michuano ya Euro 2020 huko St. Petersburg.
Mostovoy alijumuishwa katika kikosi cha Urusi mwaka jana. Alicheza mechi nane kati ya 11 za mwisho za timu hiyo kama mchezaji wa akiba. Ujerumani, Ufaransa na Ureno Kundi moja Euro 2020
Mechi pekee aliyocheza Evgeniev katika timu ya taifa ilikuwa ni dhidi ya Serbia ambapo Urusi ilipoteza kwa kufungwa mabao 5-0 mwaka jana.
Sweden na Uhispania pia zimeripoti visa vya wachezaji kupata maambukizi ya corona lakini bado hazijachukua uamuzi wa kuwabadilisha wachezaji walioathirika.
AP