1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiIraq

Meya na maafisa watano wafukuzwa kwa vifo vya watu 107 Iraq.

2 Oktoba 2023

Mamlaka nchini Iraq imesema meya na mkuu wake wa zimamoto ni miongoni mwa maafisa watano wa taifa hilo waliofutwa kazi kwa kile kilichoelezwa kuwa uzembe mkubwa baada ya ajali ya moto iliyoua watu 107.

Irak Feuer in einem Hochzeitssaal
Picha: ZAID AL-OBEIDI/AFP/Getty Images

Mamlaka nchini Iraq imesema meya na mkuu wake wa zimamoto ni miongoni mwa maafisa watano wa taifa hilo waliofutwa kazi kwa kile kilichoelezwa kuwa "uzembe mkubwa" baada ya ajali ya moto ya wiki iliyopita ulioua watu 107 kwenye harusi.

Duru zinaeleza pamoja na kushtakiwa kwa uzembe meya huyo atashitakiwa kwa kuruhusu ujenzi holela wa jengo kulikotokea maafa hayo.

Mkasa huo ulitokea katika mji wa kaskazini mwa Iraq wa Qaraqosh, sehemu ya jamii ndogo ya Wakristo wa Iraq karibu na Mosul, katika ukumbi wa harusi uliokuwa na uwezo wa kuchukua takriban watu 400.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW