Janga
Moto na milipuko kambi ya kijeshi Burundi vyaua watu 13
2 Aprili 2026
Matangazo
Jeshi limesema moto huo ulizuka usiku katika ghala la kuhifadhia vifaa vya kijeshi na kusababisha milipuko kadhaa baada ya risasi na mabomu kulipuka.
Msemaji wa jeshi, Gaspard Baratuza, amesema chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme, akisisitiza kuwa hakukuwa na shambulio lolote dhidi ya kambi hiyo.
Tukio hilo lilitokea katika eneo la Musaga, nje kidogo ya jiji la Bujumbura, ambapo wakazi walikimbia kwa hofu huku milipuko ikisikika kwa umbali mkubwa.
Maafisa wamewataka wananchi kutoa taarifa kuhusu mabaki ya milipuko ambayo hayajalipuka, wakati hali ikianza kurejea kawaida.