1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaPeru

Moto ulozuka mji mkuu wa Peru waendelea kuwaka

6 Machi 2025

Mamia ya wazima moto wanapambana kuuzima moto mkubwa unaowaka kwenye majengo kadhaa katikati mwa mji mkuu wa taifa la Amerika ya Kusini la Peru, Lima, kwa siku ya pili mfululizo.

Moja ya mitaa ya mji mkuu wa Peru, Lima.
Moja ya mitaa ya mji mkuu wa Peru, Lima.Picha: Stefan Zeitz/Geisler-Fotopress/picture alliance

Moto huo ulizuka siku ya Jumatatu kwenye bohari moja iliyokuwa ikiendeshwa bila vibali katika wilaya ya Barrios Altos. Idara ya Zimamoto imesema moto huo ulisambaa kutoka jengo hilo kwenda mengine ambapo tangu wakati huo majengo manne yameungua na kuporomoka.

Mkuu wa idara hiyo Carlos Malpica amesema kukosekana kwa miundombinu ya kusambaza maji kumeongeza wasiwasi kuwa moto huo utaendelea kuwaka kwa siku kadhaa zinazokuja.

Familia kadhaa zimehamishwa kutoka nyumba zinazowaka moto, huku watu wengi wakijaribu kuondoka na majokofu, viti na magodoro.

Hakuna majeruhi wala kifo kilichoripotiwa hadi sasa lakini kiongozi wa manispaa ulikotokea moto huo amesema familia nyingi zimepoteza mali.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW