Moto wa nyika wawaua watu 51 huko Chile
4 Februari 2024Idadi ya vifo kutokana na moto mkali wa mwituni nchini Chile imeongezeka hadi kufikia 51huku rais Gabriel Boric akisema idadi ya vifo inatarajiwa kuongezeka. Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo Carolina Tohá amesema maelfu ya nyumba zimeathirika pakubwa kufuatia moto huo.
Moto huo umejikita katika maeneo ya watalii ya Vina del Mar na Valparaiso, ambapo umeharibu mamia ya hekta za misitu na kuwalazimisha watu kuhama. kulingana na CONAF, mamlaka ya kitaifa ya misitu ya Chile hadi siku ya Jumamosi ilikuwa imerekodi visa 143 vya moto nchini humo na kuhusisha eneo la takriban hekta 21,000. katika eneo la Valparaiso nyumba takriban 3000, zimeteketea kwa moto.
Rais Boric alitangaza "hali ya hatari kutokana na maafa, ili kuwa na rasilimali zote muhimu" za kukabiliana na moto huo na kuiagiza wizara ya Ulinzi kupeleka zaidi vitengo vya kijeshi.