1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAsia

Ajali ya moto yauwa 32 kwenye mgodi wa chuma Kazakhstan

28 Oktoba 2023

Watu wasiopungua 32 wamekufa leo baada ya moto mkubwa kuzuka kwenye mgodi wa chuma nchini Kazakhstan, mkasa uliolazimisha serikali kutangaza mpango wa kusitisha ushirikiano na kampuni inayoendesha mgodi huo.

Mgodi wa kampuni ya ArcelorMittal uliokumbwa na ajali ya moto
Mgodi wa kampuni ya ArcelorMittal uliokumbwa na ajali ya motoPicha: Ruslan Pryanikov/AFP

Hadi sasa hakuna sababu iliyotolewa juu ya chanzo cha moto huo lakini kiasi waokoaji 40 wametumwa kwenda kuwatafuta wachimbaji wengine 23 waliokuwa ndani ya mgodi wakati mkasa huo ulipotokea.

Mgodi huo ulio karibu na mji wa mkoa wenye shughuli nyingi za viwanda wa Karaganda unaopatikana katikati mwa Kazakhstan, unamilikiwa na kampuni kubwa ya uchimbaji chuma ya ArcelorMittal.

Kampuni hiyo meandamwa na mfululizo wa matukio ya ajali za aina hiyo kutokana na kile maafisa wa Kazakhstan wanasema kwamba inatokana na tabia ya kupuuza kanuni za usalama. Kufuatia mkasa wa leo rais Kassym-Jomart Tokayev ameamuru serikali isitishe mara moja uwekezaji wa kampuni hiyo na ianze mchakato wa kuibinafsisha.