1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Moto wazuka katika shule ya wasichana ya Isiolo, Kenya

8 Septemba 2024

Moto ulizuka katika shule ya upili ya wasichana ya Isiolo nchini Kenya jana Jumamosi na kusababisha kujeruhiwa kwa wanafunzi watatu na kuharibika kwa mali. Haya ni kwa mujibu wa Shirika la Msalaba Mwekundu na polisi.

Moto wateketeza bweni katika shule  ya msingi ya HillsideEndarasha katika kaunti ya Nyeri mnamo Septemba 6.2024
Moto wateketeza bweni katika shule ya msingi ya HillsideEndarasha katika kaunti ya NyeriPicha: AP Photo/picture alliance

Katika chapisho jana jioni katika mtandao wa X, shirika hilo lilithibitisha kisa hicho na mapema leo limesema kuwa moto huo umedhibitiwa.

Msemaji wa polisi nchini humo, Resila Onyango, pia alisema jana kuwa moto huo ulidhibitiwa ijapokuwa hakuelezea chanzo chake.

Juhudi ya kutafuta wanafunzi na kuokoa mali zandelezwa

Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa muda mfupi baada ya moto huo kuzimwa, polisi, vikosi vya zimamoto na vya uokoaji vilionekana vikitumia tochi kutafuta wanafunzi na kuokoa mali katika mabweni yaliyoteketea.

Moto huo unafuatia vifo vya takriban wanafunzi 21 katika shule ya msingi ya Hillside Endarasha mjini Nyeri, mapema Ijumaa baada ya bweni moja kuteketea shuleni humo.