Mourinho: Terry atachezea Chelsea msimu ujao
6 Machi 2015Matangazo
Terry mlinzi wa kati mwenye umri wa miaka 34 ana mkataba wa mwaka mmoja utakaomalizika mwishoni mwa msimu huu. Mourinho aliuambia mkutano na waandishi wa habari Jumatano kwamba anajuwa anachoambiwa na bodi ya kilabu na kile anachoambiwa na wachezaji wake na hakuna shaka yoyote Terry atapewa mkataba mpya kabla ya mwisho wa msimu huu na hilo anauhakika nalo. Mourinho akaongeza kwamba, utafika wakati kwa Chelsea kufikiria nania atajaza pengo litakaloachwa na Terry, lakini wakati huo bado haujafika.
Mwandishi: Mohammed Abdul-Rahman
Mhariri: Josephat Charo