Mpaka kati ya DRC na Burundi wafunguliwa
23 Februari 2026
Matangazo
Mpaka kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Burundi umefunguliwa tena hivi leo Jumatatu baada ya kufungwa kwa zaidi ya miezi miwili.
Taarifa hiyo imethibitishwa na maafisa wa Kongo na polisi wa Burundi ambao wamezungumza na shirika la habari la AFP.Maelfu ya Wakongo wakimbilia Burundi baada ya M23 kuudhibiti mji wa Uvira
Vyanzo vyote hivyo vimesema mpaka wa Kavimvira ambao unatumiwa zaidi kwa shughuli za kibiashara na ambao ulifungwa mwezi Desemba kufuatia operesheni ya kundi la waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda, ulifunguliwa mapema leo asubuhi.