MPALESTINA APIGWA RISASI NA ISRAEL
16 Novemba 2003Matangazo
GAZA: Mpalestina mmoja ameuawa baada ya kupigwa risasi na vikosi vya Israeli mapema asubuhi ya leo kusini mwa Ukanda wa Gaza.Mtoto wa kiume wa miaka 8 alijeruhiwa katika opresheni hiyo iliyoanza kabla ya alfajiri.Kwa mujibu wa mashahidi na duru za tiba nyumba moja pia iliteketezwa.Jeshi la Israel limethibitisha kuwa mtu mmoja alipigwa risasi katika opresheni ya kutaka kumkamata Mpalestina mmoja.
