1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mpango wa bahati nasibu wa uhamiaji Marekani wasimamishwa

19 Desemba 2025

Waziri wa usalama wa ndani wa Marekani, Kristi Noem, ameusimamisha mpango wa bahati nasibu wa uhamiaji, "Green Card Lottery" akisema mpango huo ulitumika na mtuhumiwa wa shambulio la risasi katika Chuo Kikuu cha Brown.

Marekani  2023 | Green Card | Uhamiaji
Mpango wa bahati nasibu wa uhamiaji Marekani "Green Card Lottery"Picha: Mehaniq/Panthermedia/IMAGO

Waziri wa usalama wa ndani wa Marekani Kristi Noem ameandika kwenye mtandao wa kijamii kwamba mshukiwa huyo, Manuel Neves Valente, aliingia Marekani kupitia mpango wa bahati nasibu ya viza ya uhamiaji mnamo mwaka 2017 na baadae kupewa kibali cha kuishi na kufanya kazi nchini humo.

Amesema ameusimamisha mpango huo ili kuhakikisha hakuna Wamarekani zaidi watakaodhurika.

Claudio Neves Valente, raia wa Ureno mwenye umri wa miaka 48, anaripotiwa kuvamia jengo la chuo kikuu cha Brown mnamo Desemba 13 na kufyatua risasi kwa wanafunzi waliokuwa wakifanya mitihani, na kusababisha vifo vya watu wawili na kuwajeruhi wengine tisa.

Kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, mpango wa bahati nasibu ya uhamiaji hutoa hadi viza 55,000 kila mwaka kwa watu "kutoka nchi zenye viwango vya chini vya uhamiaji kwenda kuishi na kufanya kazi Marekani."

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW