EU na A. Mashariki kuboresha zaidi upatikanaji masoko, Ulaya
6 Oktoba 2023Mpango huo wa kuboresha upatikanaji masoko kwa wafanyabiashara wadogo barani Ulaya, unajulikana kama MARKUP II na utagharimu yuro milioni 40.
Katika uzinduzi wa mpango huo uliofanyika makao makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Arusha Tanzania, Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini humo Christine GRAU, pamoja na mambo mengine amebainisha kwamba dhamira ya Umoja wa Ulaya ni kusaidia makampuni ya Afrika Mashariki kupanuka kibiashara na kutoa ajira kwa vijana.
Kulingana na Katibu mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dr. Peter Mathuki, awamu hii ya pili itawajumuisha wanawake na vijana katika biashara, huku wizara husika kutoka serikali za nchi wanachama zikitarajiwa kutoa mwelekeo wa jumla wa kuendesha mpango huo, unaotoa kipaumbele kwa mazao ya kilimo kama vile Parachichi, Kakao, maharagwe na Chai.
Awamu ya kwanza ya mpango huo iliyanufaisha takribani makampuni 700 ya kikanda na kuwezesha upatikanaji wa Dola zaidi ya milioni 10 za kimarekani.
Sikiliza pia: