Mpango wa waomba hifadhi wa Uingereza watarajiwa kuwa sheria
18 Julai 2023Mpango wa waziri mkuu wa Uingereza Rishi Sunak uliokumbwa na upinzani mkubwa, wa kurahisisha kuwapeleka waomba hifadhi nchini Rwanda, unatazamiwa kuwa sheria baada ya serikali kushinda majaribio ya baraza la juu la bunge kuufanyia mabadiliko mswada wa sheria yake.
Mabadiliko ya mwisho mswada yamepigiwa kura leo
Mswada huo ulikuwa umekwama katika majibizano makali kati ya bunge la kuchaguliwa na baraza la juu lisilo la kuchaguliwa, ambalo mara kadhaa lilifanya mabadiliko katika sheria hiyo ili kupunguza makali yake. Mapema leo asubuhi mabadiliko ya mwisho yalipigiwa kura ya HAPANA. Baadae utapelekwa kwa Mfalme Charles III kwa ajili ya kuidhinishwa kuwa sheria.
Kuidhinishwa kwa sheria hiyo kutazuia kusafirishwa kwa waomba hifadhi
Kuidhinishwa kwa sheria hiyo kutaizuiwa serikali ya Uingereza kuwasafirisha waomba hifadhi hadi nchi inayoiitwa salama kama Rwanda au katika mataifa yao asili. Umoja wa Mataifa imeikosoa sheria hiyo na kuitaja kuwa inakwenda kinyume na sheria ya kimataifa.