1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaRwanda

Mpango wa Uingereza, Rwanda wa wahamiaji wakumbwa na kikwazo

Daniel Gakuba
17 Januari 2023

Korti mbili za rufaa mjini London ziliamua hapo jana kuwa pingamizi la kisheria linaweza kuwekwa dhidi ya mpango wenye utata wa serikali ya Uingereza wa kuwahamishia waomba hifadhi nchini Rwanda.

Großbritannien Protest gegen die Abschiebung von Geflüchteten zurück nach Ruanda
Picha: Niklas Halle'n/AFP/ Getty Images

Mwezi uliopita Mahakama ya Juu ya nchi hiyo ilitoa hukumu yake iliyohalalisha mpango huo unaolenga kupunguza idadi ya watu wanaotimia njia ya bahari kuingia Uingereza wakitokea barani Ulaya. Uamuzi wa jana unalipa shirika la hisani la kuwasaidia wahamiaji la Asylum Aid, kuitaka Mahakama ya Rufaa kutafakaa upya vipengele vya hukumu ya Mahakama ya Juu.

Mojawapo ya vipengele hivyo ni ikiwa majaji wa Mahakama ya Juu walifnya kosa katika kuamua kwamba kulikuwapo hakikisho la kutosha, la kuzuia kuwapeleka waomba hifadhi katika nchi ambapo wanaweza kukabiliwa na vitisho. Shirika hilo pia linaweza kutoa hoja kuwa mpango mzima huo wa Uingereza sio sahihi kimfumo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW