Mpizani wa Cameroon asema madikteta hawataki maandamano
22 Septemba 2020Mkosoaji huyo mkubwa wa serikali anadai kuwa rais wa muda mrefu Paul Biya ajizulu na kuruhusu yafayike mageuzi ya sheria za uchaguzi. Katika mahojiano maalum na DW, Kamto anazungumzia juu ya maandamano na maono yake kwa ajili ya taifa hilo lenye matatizo la Afrika ya kati.
Alipoulizwa kuhusu kile anachotaka kufanikisha kupitia maandamano hayo, Maurice Kamto alisema , kuna kuna mambo mawili makuu. La kwanza ni kusitisha mara moja umwagaji damu katika eneo la kaskazini magharibi na kusini magharibi kwa njia ya kusitisha mapigano. Unaweza kufanikisha usitishaji mapigano kwa njia mbili tofauti. Ama majeshi ya taifa , jeshi la Cameroon , linalazimika kuwa na mawasiliano na kundi lenye silaha na kukamilisha usitishaji mapigano. Ama wanaweza kutangaza wenyewe tu kusitisha mapigano na kuangalia iwapo makundi yenye silaha yatatekeleza makubalinao hayo ya kusitisha mapigano ama la.
Nafikiri ni njia nzuri kufanya hivyo haraka. Iwapo hawataki kuonekana kuwa ni dhaifu, kwasababu wanajaribu kujadiliana na makundi yenye silaha, , wanaweza tu kusema kwa wiki mbili zinazokuja, tutayarejesha majeshi yetu katika kambi, na tutaona jinsi makundi yenye silaha yatakavyochukua uamuzi.
Hii kwetu na mimi, ni njia bora kabisa ya kufanikisha usitishaji mapigano na kuzuwia umwagikaji wa damu na vita vya kijinga katika eneo la kaskazini magharibi na kusini magharibi mwa Cameroon.
Mfumo wa uchaguzi
Nafasi ya pili ni mageuzi ya mfumo wa uchaguzi kwasababu tumekuwa tukitekeleza mfumo wa sasa wa uchaguzi tangu mwaka 2012 na tumeweza kupata matokeo yale yale, ikiwa na maana kupingwa kwa matokeo ya uchaguzi. Ndio sababu hatukuweza kuingia katika uchaguzi wa Februari mwaka 2020 kwasababu njia ile ile itatoa matokeo yale yale. Hadi pale utakapobadilisha mfumo wa uchaguzi, tutakuwa na matokeo yale yale kila wakati tunapotayarisha uchaguzi nchini Cameroon.
Umewahi kuona wapi utawala wa kidikteta ukiyaona maandamano kama ni haki ya kisheria? Maurice Kamto alijibu hivyo baada ya kuulizwa kwamba anazungumzia kuhusu kuzuwia umwagaji damu, na maafisa nchini humo wanasema maandamano ni kinyume na sheria na kwamba majeshi ya usalama , "yatachukua hatua zote stahili kuweka utulivu na kulinda sheria."
Maandamano
Haoni kwamba anawaweka waungaji wake mkono katika hatari? Kamto alisema ni sheria gani ambayo inakiukwa kwa kufanya maandamano ? Katiba ya Cameroon iko wazi kabisa kuhusu hilo. Uhuru wa kukusanyika, kuhutubia, na maandamano kwa mujibu wa sheria.
Ina maana kwamba unatekeleza kwa mujibu wa sheria, na sio kwamba sheria ama maafisa wa utawala wanaweza kupiga marufuku uhuru uliomo katika katiba. Mwishoni mwa hayo, katiba hiyo hiyo inasema kwamba serikali itahakikisha kila mtu anatumia sheria hizi zinazomhusu kila raia. Kwa hiyo hakuna ukiukaji wa sheria yoyote hapo.
Unapozungumzia watu kuwaweka katika hatari , ni ujumbe wa jeshi ama serikali kufyatulia watu risasi ambao wanataka kuandamana kwa amani ? Tunafikiri kwamba njia pekee kwetu kueleza kutokubaliana , hasira zetu, mfadhaiko wetu kwa serikali hii ni kuandamana kwa amani. Kwa kuwa hatuwezi kufanya kupitia uchaguzi ulio huru na wa haki, hatutaweza kwenda barabarani kucheza. Tunakwenda huko kwasababu tuko na furaha kwenda huko. Tungependa kusisisitiza hilo.