1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mradi wa maendeleo kufanikiwa nchini Mali

R.Maack/M.Dreyer24 Agosti 2005

Wakati msiba wa njaa unaziathiri nchi za Niger na Mali, shirika la kutoa misaada ya maendeleo linaridhika na kazi yake katika eneo la Kusini mwa nchi ya Mali. Tangu miaka 11 shiriki hilo linaloitwa kwa ufupi GTZ linaungana na wananchi wa sehemu hii kusini mwa mji wa Timbuktu katika jangwa la Sahara.

Mtuareg aliyerudi nchini Mali
Mtuareg aliyerudi nchini MaliPicha: AP

Wakati huo watu walikuwa wamelikimbia eneo hili kwa sababu ya ukame kubwa pamoja na vita vya watu wa kabila la Tuareg. Serikali ya Mali iliiomba serikali ya Ujerumani kuisaidia kumaliza mzozo na kabila la Tuareg. Watuareg ambao ni wahamahamaji wanaoishi katika jangwa walikuwa wakipinga serikali ya Mali inayokaa mjini Bamako, kusini mwa nchi hiyo kwa sababu hawana wakilishi wowote ndani ya serikali. Baada ya kusainiwa katiba ya amani na vikundi mbali mbali ya vita, serikali ya Ujerumani imetuma shirika lake la kutoa msaada kuanza kazi yake katika eneo hili la vita lililoachiwa kabisa. Sasa watu millioni 1,5 wanapoishi tena. Yahia Ag Mohammed Ali, ambaye ni mratiba wa mradi wa GTZ, anaeleza vipi shirika hili liliendesha shughuli za maendeleo katika eneo la kaskazini mwa nchi hii ya Mali:

„Wajerumani walisema: Sisi tunataka tu kuwasaidia watu kutatua matatizo ambayo hawawezi kuyatatua wenyewe. Wale waliorudi kwenye mahali walipozaliwa walipewa mabomba ya maji, majengo ya shule, hospitali na mifugo. Lakini Wajerumani hawakufanya maamuzi yoyote. Badala yake walianza majadiliano baina ya makabila mbali mbali juu ya maisha yao ya pamoja.“

Kwa kujishughulisha sana binafsi, wafanyakazi wa GTZ walijaribu kupatanisha baina ya Watuareg na makabila ya Kiafrika yaliopigana hapo zamani na kupunguza hali ya kutoaminiana baina yao. Shughuli hizi zilianza kwa majadiliano ya kununua punda,hadi kufikia vipi kuuza na kusafirisha bidhaa. Hali ya amani katika eneo hili ni yenye uwezekano wa kuvunjika upesi. Wengine wanapinga mradi wa GTZ. Wanasema kwamba kiongozi wa Kijerumani wa mradi huo anatawala kama mfalme – akiondoka hali ya amani itavunjika.

Lakini mradi wa GTZ umefanikiwa: Wakimbizi walirudi nyumbani, na kuna amani. Hata hivyo shirika la GTZ linaendelea na kazi yake. Sasa linajishughulika na tatizo la kumwagilia maji mashamba kwa ajili ya kilimo. Hii ni kazi kubwa, anasema Yahia Ag Mohammed Ali: „Suala la ardhi ndiyo lina uwezekano kubwa wa kuanzisha mzozo. Mara nyingi watu wanagombana kwa sababu ya ardhi na ni lazima kulitatua kabisa tatizo hili.“

Zaidi ya millioni 50 za dola za Kimarekani zimelipwa na GTZ kwa ajili ya mradi wake Kaskazini mwa Mali. Bw. Yahia anadhani kwamba fedha hizi zilitumika vizuri, kwa sababu iliboresha maisha ya watu wa huko. Anasema kwamba kulingana na wakati wa vita tofauti ni kubwa kabisa. Mwaka huu mavuna yalikuwa mbaya kutokana na ukame pamoja na balaa la nzige. Hata hivyo watu wanaweza kuishi kwa sababu ya mradi wa kumwagili maji. Bila ya huo palikuwa na njaa na magipano, anaona Mmali Yuhia Ag.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW