130709 Nabucco Pipeline Ankara
13 Julai 2009Katika juhudi za kuepuka matatizo ya ugavi wa gesi kutoka Urusi, nchi nne za Umoja wa Ulaya pamoja na Uturuki zimetiliana saini makubaliano juu ya ujenzi wa bomba la gesi kutokea bahari ya Caspian .
Mradi huo unatazamiwa kumalizika mnamo mwaka 2014. Lakini pana maswali ya kuuliza.
Jee Fedha zitatoka wapi, ili kuutekeleza na gesi yenyewe itatoka wapi ?
Uturuki na nchi nne za Umoja wa Ulaya leo zimetiliana saini leo makubaliano juu kutelekeza mradi wenye lengo la kuziwezesha nchi za Ulaya kupunguza kuitegemea Urusi kwa mahitaji yao ya gesi. Mradi huo ni wa kujenga bomba la gesi litakalopitia katika nchi hizo tano kutokea bahari ya Caspian kwa kuikwepa Urusi.
Nchi hizo ni Austria, Hungary, Romania,Bulgaria na Uturuki.
Waziri mkuu wa Uturuki Erdogan amesema leo kwenye sherehe ya kutiliana saini mjini Ankara , kwamba msingi wa kuanza kujenga bomba hilo umeshawekwa.Bomba hilo la gesi litakalokuwa na urefu wa kilometa 3300 linatazamiwa kukamilika mnamo mwaka 2014. Gesi kiasi cha kubik meta bilioni 31 kitapitia katika bomba hilo litakalopitia katika nchi hizo tano.Mazungumzo juu ya mradi wa bomba hilo unaoitwa Nabucco yalianza kufanyika mwaka 2002.
Waziri Mkuu wa Bulgaria Sergei Stanichew alietia saini mkataba wa mradi wa Nabucco kwa niaba ya nchi yake amesema nchi zao bado ziko mbali kukamilisha mradi wa Nabucco kwa miaka kadhaa lakini kwa serikali ya Bulgaria na kwa watu wa nchi yake waliokabiliwa na hali mbaya sana wakati wa mgogoro wa nishati katika mwezi januari, hatua ya kutiwa saini mkataba huuleo, ni ujumbe madhubuti kisiasa na kiuchumi.
Hatahivyo bado pana maswali yanayopaswa kujibiwa juu ya mradi wa Nabucco; kwa mfano gesi inayokusudiwa kuletwa barani Ulaya kwa kupitia katika nchizilizotia saini leo itatoka wapi? Mpaka sasa ni Azerbaijan tu inayoonekana kuwa mgavi imara wa gesi hiyo.
Swali jingine linahusu fedha za kugharamia mradi huo wa Euro bilioni nane.Umoja wa Ulaya hadi sasa umeahidi Euro milioni 250 tu.
Mwandishi/Kilian Pfeffer.
Mfasiri Mtullya. A.
ZA.