1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mripuko wa kituo cha mafuta wauwa 20 Nagorno-Karabakh

26 Septemba 2023

Takriban watu 20 wamekufa na wengine karibu 300 wamejeruhiwa baada ya kutokea mripuko katika kituo kimoja cha mafuta huko jimboni Nagorno-Karabakh.

Aserbaidschan | Rauch nach der Explosion eines Tanklagers
Picha: Nagorno-Karabakh Human Rights Ombudsman/AFP

Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa wizara ya afya ya eneo linalozozaniwa la Kaukasi ya Kusini. Baada ya mripuko huo uliotokea jioni ya Jumatatu, majeruhi walioplekwa hospitali wanaelezwa kuwa na majeraha ya viwango tofauti.

Hadi wakati huu bado, haijaweza kufahamika ni nini hasa kilisababisha ajali hiyo iliyotokea katika eneo lenye idadi kubwa ya jamii ya Waarmenia, ambao kwa duru za juma lililopita lilishindwa katika makabiliano ya kijeshi na Azerbaijan.

Miili ya watu 13 imeteketekea kwa moto.

Kufikia Asubuhi ya Jumanne hii, tayari watu 7 ambao walifikishwa katika kituo cha afya waliripotiwa kupoteza maisha. Wizara ya afya ilisema miili mingine ya watu 13 iliopolewa kutoka katika eneo la ajali. Hata hivyo hata idadi hiyu ya watu ambao wamejeruhiwa wengi wao wapo katika hali ya umaututi. Muda mfupi baada ya ajali, katika ripoti za awali kabisa serikali ilisema takribani watu 200 wamejeruhiwa.

Wakazi wa Nagorno wakikimbilia ArmeniaPicha: Gayane Yenokyan/AP Photo/picture alliance

Katika mitandao ya kijamii, kumetapakaa picha zenye kuonesha moto mkubwa uliozuka katika eneo hilo. Mwanasiasa Metakse Akopyan amesema wakati ajali hiyo ikitokea idadi kubwa ya watu ilikuwa katika foleni ya kutaka kujipatia mafuta ya kwa lengo la kukimbilia Armenia kwa usafiri wa gari.

Wakaazi wa Nagorno Karabakh wanakimbilia Armenia baada ya Azerbaijan kufanya operesheni kabambe ya kijeshi ya kulirejesha kikamilifu eneo hilo baada ya miongo mitatu mamlaka iliyojitenga. Kutokana na hali ilivyo sasa.

Wito wa kulinda haki za wakazi wa Nagorno-Karabakh

Mkuu wa shirika la misaada la Marekani la USAID Samantha Power anasema "Kwanza kabisa, tunatoa wito kwa Azerbaijan kudumisha usitishaji wa vita na kuchukua hatua madhubuti kulinda haki za raia huko Nagorno-Karabakh. Rais Aliyev ameahidi kulinda haki za raia wa jamii ya Warmenia. Azerbaijan lazima itimize ahadi hiyo."

Ofisi yenye dhima ya haki za binadamu katika eneo hilo imetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kufanya juhudi za haraka za kuwasaidia manusura, ikisema kuha uhitaji wa dharura la kuwasafirisha watu nje ya eneo hilo kwa matibabu zaidi na hasa wale waliojeruhiwa vibaya. Na ikielezwa pia uwezo wa kutoa huduma  kwa majeruhi kwa ndani Nagorno-Karabakh ni mdogo.

Katika operesheni ya kijeshi ya kasi iliyodumu kwa takribani masaa 24, ya juma lililopita, jeshi la Azerbaijani, lilifanikiwa kuwalazimisha wapiganaji wa mamlaka waliojitenga kuweka chini mtutu wa bunduki na kuanza mazungumzo yenye kuhusu  "kuunganishwa tena" kwa Nagorno-Karabakh, huku Azerbaijan ikitoa ahadi ya kuheshimu jamii ya wakazi wa Armenia katika eneo hilo.

Soma zaidi:Mzozo kati ya Armenia na Azerbaijan imekuwa ukijirudia mara kwa mara katika jimbo la Nagorno-Karabakh

Kauli hiyo pia ilikwenda sambamba na ahadi ya kurejesha uhuduma za msingi baada ya kuwekewa vikwazo kwa takribani miezi 10. Hata hivyo wakazi wengi walihofia kulipiziwa visasi na hivyo kukimbilia Armenia. Serikali ya Armenia ilisema kuwa zaidi ya watu 6,500 wa Nagorno-Karabakh wameingia Armenia hadi jana usiku.

Vyanzo: DPA/AP

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW