1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiNigeria

Mripuko wa lori la mafuta waua karibu watu 100 Nigeria

16 Oktoba 2024

Msemaji wa polisi nchini humo Lawan Shiisu Adam amesema hadi sasa wamethibitisha vifo vya watu 94 huku kionya kuwa idadi hiyo inaweza kuongezeka.

Mripuko wa lori la mafuta waua karibu watu 100 Kaskazini mwa Nigeria
Mripuko wa lori la mafuta waua karibu watu 100 Kaskazini mwa NigeriaPicha: Polícia da República de Moçambique

Polisi wameendelea kueleza kuwa wengi wa walioathiriwa walikuwa wakijaribu kuchota mafuta yaliyomwagika baada ya lori kuanguka jana jioni katika mji wa Majia jimboni Jigawa.

Chama cha Madaktari nchini Nigeria kimewataka wahudumu wa afya kuwasili haraka kwenye vituo vya dharura vilivyo karibu ili kusaidia kutoa huduma kwa idadi kubwa ya majeruhi. Ajali kama hizi zimekuwa zikitokea mara kwa mara nchini Nigeria na kusababisha vifo vya mamia ya watu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW