1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mripuko wa maradhi ya Ebola -Liberia

Isaac Gamba
24 Julai 2018

Mwanamke wa kiliberia ambaye aliambukizwa maradhi ya Ebola mwaka 2014 anaweza kuwa amewaambukizwa ndugu zake watatu mwaka mmoja baada ya kuuugua maradhi hayo.

Mwanamke wa kiliberia ambaye aliambukizwa maradhi ya Ebola mwaka 2014 anaweza kuwa amewaambukizwa ndugu zake watatu mwaka mmoja baada ya kuuugua maradhi hayo, kulingana na ripoti ya utafiti iliochapishwa katika jarida la afya la Lancet.

Kumekuwepo na visa vya awali kwa wanaume kusambaza maradhi ya Ebola kwa wanawake kupitia njia ya kujamiiana ambapo kirusi cha maradhi hayo kina weza kuishi katika manii ya mwanaume  zaidi ya mwaka mmoja lakini kisa hicho kipya ni cha mara ya kwanza wanasayansi kubaini kwamba  maradhi ya Ebola  yaliweza kusambaa kutoka kwa mwanamke baada ya kipindi hicho kirefu.

Hatua  hii ya nadra  ya kusambaa maradhi ya Ebola ikiwa ni  muda mrefu baada ya  kuambukizwa inaaashiria  umuhimu wa kufuatilia manusura wa maradhi hayo hususani katika maeneo kama  vile ya Congo.

Visa vya watu 38 tayari vimethibitishwa ikiwa ni pamoja na vifo vya watu 14 tangu mripuko wa maradhi hayo hivi karibuni uliporipotiwa mwezi Mei nchini humo. Hata hivypo mripuko huo unatarajiwa kuwa tayari umedhibitiwa siku ya Jumatano (25.07.2018) ikiwa ni siku ya 42 tangu kisa cha mwisho cha maradhi hayo kiliporipotiwa.

"Kirusi cha  Ebola hujificha  katika sehemu ambazo kinaweza kuepuka kinga za mwili hivyo kuna haja ya kuwa waangalifu zaidi," anasema Daktari David Heymann, Professor wa maradhi ya kuambukiza  katika chuo kikuu cha mjini London cha masuala ya Afya na dawa katika ukanda wa nchi za Tropiki, ambaye hakuhusishwa katika utafiti huo mpya

 

Kugundulika kwa visa vya Ebola

Visa vya maradhi hayo ambavyo si vya kawaida nchini Liberia viligundulika baada ya mvulana wa umri wa miaka 15 mtoto wa mwanamke huyo alipotibiwa maradhi hayo ya Ebola  Novemba 2015 na baadaye wataalamu kumpima mwanamke huyo, mumewe na watoto wao watatu wa kiume.

Mvulana huyo mwenye umri wa miaka 15 alifariki dunia  siku chache baadaye huku baba na mvulana mwenye umri wa miaka 8, waliokuwa tayari wameambukizwa maradhi ya Ebola wakipona  na mtoto wao wa kiume aliyekuwa na umri wa miaka mitano hakuwa ameambukizwa.

Watafiti wanaarifu juu ya kufanana kwa vinasaba kutokana na virusi vilivyokutwa katika vipimo vilivyokutwa kwenye mwili wa baba, watoto wawili na hali inayohusiana na kusambaa  virusi hivyo wakati wa mripuko wa maradhi hayo katika kipindi cha mwaka 2014- 2015 nchini Liberia, Guinea na Sierra Leone, mripuko ulioua watu 11,000 ambayo ni idadi kubwa  katika historia ya mripuko wa maradhi ya Ebola.

Wanasayansi wamebaini kwamba mwanamke huyo alikuwa tayari amemhudumia kaka yake Julai , 2014 aliyefariki baada ya kugundulika kuwa alikuwa na dalili za maradhi yanayoonekana  kama Ebola lakini kabla ya kupimwa ili kuthibitisha ukweli wa suala hilo.

Mwanamke huyo baadaye alibainika kuugua Ebola lakini hakutafuta tiba.

Wiki kadhaa baadaye baada ya kujifungua  Septemba 2015 mwanamke ahuyo alianza kuchoka ikiwa mi pamoja na kukumbwa na matatizo ya kupumua  na madaktari wanasema kutokana na uja uzito hupunguza kinga ya mwili basi hatua hiyo inaweza kusabaisha virusi vya Ebola kujitokeza.

Mwandishi: Isaac Gamba /APE

Mhariri: Iddi Ssessanga

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW