1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Mripuko waua 8 na kujeruhi 84 Guinea

18 Desemba 2023

Takriban watu wanane wameuawa na wengine 84 wamejeruhiwa kufuatia mripuko mapema leo katika bohari ya mafuta katika mji mkuu wa Guinea, Conakry.

Zentralgefängnis Guinea Conakry
Mripuko umeua watu wanane na wengine zaidi ya 80 kujeruhiwa Guinea.Picha: CELLOU BINANI/AFP

Takriban watu wanane wameuawa na wengine 84 wamejeruhiwa kufuatia mripuko mapema leo katika bohari ya mafuta katika mji mkuu wa Guinea, Conakry. Hayo yameelezwa na afisa mkuu wa polisi nchini humo ambaye amesema idadi hiyo ni ya muda na kwamba moto huo umedhibitiwa.

Soma pia: Guinea:Waandamanaji wa upinzani wasiopungua kumi wauliwa

Mlipuko katika bohari pekee ya mafuta katika taifa hilo la Afrika Magharibi, ulitikisa wilaya ya Kaloum katikati mwa jiji la Conakry, na kuwalazimisha mamia ya watu kulikimbia eneo hilo.

Moto mkubwa na moshi mweusi vilishuhudiwa hadi kwa umbali wa kilometa kadhaa huku vikosi vya zima moto vikiwasili na malori ya mafuta yakiondoka eneo hilo yakisindikizwa na polisi. Serikali ya Guinea imewataka raia wa mji mkuu kusalia majumbani mwao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW