1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Eneo lililozingirwa miezi 20 la Khartoum lapata msaada

28 Desemba 2024

Raia katika eneo lililozingirwa kusini mwa mji mkuu wa Sudan ulioharibiwa na vita wamepokea msafara wa msaada wa kiutu wiki hii ikiwa ni wa kwanza tangu vita vya taifa hilo vianze miezi 20 iliyopita.

Sudan Konvoi Humanitäre Hilfe
Serikali ya Sudan ilifanikisha msafara wa misaada ya kibinadamu kwa maelfu ya waliorejea katika Jimbo la Sinnar kusini mashariki mwa Sudan na mji wa Omdurman, kaskazini mwa mji mkuu wa Sudan Khartoum.Picha: Mohamed Iyssa/picture alliance

Sehemu ya mtandao wa kujitolea unaoratibu juhudi za msaada katika maeneo ya vita kwa taifa hilo imesema jumla ya malori 28 yaliwasili katika eneo la Jebel Awliya, kusini mwa Khartoum. Msafara huo ulijumuisha malori 22 yaliyokuwa yamebeba chakula kutoka kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), lori moja kutoka Shirika la Madaktari Wasio, na malori matano yaliyosheheni dawa kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF. Mashrika ya ndani na UNICEF wamesema vifaa hivyo vitasaidia kukidhi "mahitaji ya dharura ya afya na lishe ya watoto na familia zinazokadiriwa kufikia 200,000". Jebel Awliya ni moja kati ya maeneo mengi nchini Sudan yanayokabiliwa na njaa kubwa baada ya pande zinazozozana kuzuia barabara. Tangu vita vilipoanza Aprili 2023 kati ya jeshi la Sudan na Vikosi vya RSF, hakuna kilichoingia au kutoka bila idhini ya pande zote mbili.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW