1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Msafara wa misaada ya kibinadamu washambuliwa Butembo

2 Julai 2024

Msafara wa misaada ya kibinaadamu umeshambuliwa katika mkoa wa Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Jamhuri wa Kidemokrasia ya Kongo Kibumba 2022 | Waasi wa M23
Waasi wa M23 wakiwa wamesimama na silaha zao mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Disemba 23, 2022.Picha: Moses Sawasawa/AP Photo/picture alliance

Haya ni kwa mujibu wa shirika la Uingereza la Tearfund, ambalo kupitia taarifa yake, limesema wafanyakazi wawili bado hawajulikani walipo baada ya shambulizi hilo.

Msafara huo ulikuwa ukitoka katika eneo la mapigano na kuelekea kaskazini kabla ya kushambuliwa karibu na mji wa Butembo katika eneo la Lubero na vijana walioshukiwa kuwa waasi wa M23.

Aidha Shirika la msaada la Tearfund limesema magari yao yalichomwa na kuharibiwa katika shambulizi hilo huku wakitoa wito kwa pande zote kuheshimu na kulinda wafanyakazi wa misaada na kuhakikisha usalama wao wanapotekeleza majukumu yao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW