Msako mkali waendeshwa mjini Nairobi
10 Aprili 2014Matangazo
Kufuatia msako huo, mamia ya washukiwa wamekamatwa na polisi na wengi wanazuiwa katika ukumbi wa Kasarani kwa kukosa vibali vya kuwemo nchini Kenya kihalali miongoni mwa makosa mengine. Mashirika ya kutetea haki za binadamu na viongozi kutoka jamii ya wasomali wameishutumu sana hatua hiyo ya serikali. Hapo jana wizara ya usalama ilitangaza kuwa raia 83 wakisomali ambao hawakuwa na vibali wamerejeshwa Somalia. Caro Robi amezungumza na msemaji wa shirika la kushughulikia maslahi ya wakimbizi UNHCR nchini Kenya Emmanuel Nyabera na kwanza alimuuliza mtazamo wa shirika hilo kuhusu zoezi hilo linaoloendeshwa na Kenya. Kusikiliza mazungumzo hayo bonyeza alama ya spika za masikio hapo chini.
Mwandishi:Caro Robi
Mhariri: Josephat Charo