Msalaba Mwekundu kujadili ukiukwaji wa sheria za kimataifa
22 Septemba 2025
Matangazo
Katika taarifa ya pamoja iliyotolewa Jumapili pamoja na Brazil, China, Ufaransa, Jordan, Kazakhstan na Afrika Kusini, ICRC imezitaka nchi na jumuia ya kimataifa kuchukua hatua ili kudhibiti ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa za kibinadamu.
Taarifa hiyo imesema ulimwengu hauwezi kukaa kimya bila kufanya lolote, kwani kanuni za kimsingi za sheria ya kimataifa ya kiutu zinakiukwa mara kwa mara na kwa makusudi.
Mwaka uliopita, ICRC ilizindua mpango na nchi sita kuhimiza uungwaji mkono wa kisiasa wa sheria ya kimataifa ya kibinaadamu.
Hata hivyo, taarifa hiyo haijautaja mzozo wowote ule, ikisema inazungumzia mizozo yote ulimwenguni, inaangazia wadau wote wanaohusika, na inalenga kuhakikisha matumizi sawa ya sheria ya kimataifa ya kibinaadamu.