1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

'Msalaba Mwekundu' yaacha kutafuta wahanga wa mafuriko DRC

24 Mei 2023

Shirika la Msalaba Mwekundu lasitisha kuwatafuta wahanga wa mafuriko Kongo.

Demokratische Republik Kongo Überschwemmungen
Picha: GLODY MURHABAZI/AFP

Shirika la Msalaba Mwekundu la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo limesitisha shughuli ya kuwatafuta mamia ya wahanga wa mafuriko ya hivi karibuni mashariki mwa nchi hiyo.

Hatua hiyo imefikiwa kutokana na kukosekana kwa mashine zinazohitajika kuchimba tope na vifusi.

Wafanyakazi wa shirika hilo wamekuwa wakiitafuta miili tangu mwanzoni mwa mwezi Mei, baada ya vijiji vya Bushushu na Nyamukubi katika jimbo la Kivu Kusini kuharibiwa na mafuriko yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 460.

Mkuu wa Shirika la Msalaba Mwekundu Kivu Kusini, Desire Yuma Machumu amesema kiasi cha uchafu hakiwaruhusu kuendelea kufanya kazi kwa kutumia mikono.

Amesema shughuli ya kuwatafuta wahanga inaweza ikaaza tena iwapo maafisa wa jimbo watafanikiwa kuwapatia mashine zinazotumika kuchimba.

Gavana wa Kivu Kusini, Theo Ngwabidje Kasi, amesema barabara kuelekea kwenye vijiji bado zimeharibiwa, lakini zitafunguliwa tena hivi karibuni.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW