1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiAfrika Kusini

Msanii maarufu Afrika Kusini auawa kwa kufyatuliwa risasi

11 Februari 2023

Mmoja wa wasanii wa miondoko ya kufoka maarufu "rap" nchini Afrika Kusini, Kiernan Forbes, anayejulikana kama AKA, ameuawa jana usiku kwa kupigwa risasi nje ya mgahawa ulioko kusini mashariki mwa jiji la Durban.

Südafrika Rapper Kiernan Forbes AKA
Picha: RAJESH JANTILAL/AFP

Msanii huyo mwenye umri wa miaka 35 alishinda tuzo nyingi za Afrika Kusini na kuteuliwa mara kadhaa kwa Tuzo ya Black Entertainment Television (BET) nchini Marekani, na aliwahi kuteuliwa kwa Tuzo ya Muziki ya MTV barani Ulaya. 

Sababu ya kupigwa risasi haijafahamika na polisi wametaja kuanzisha uchunguzi. Mashambulizi ya risasi ni jambo la kawaida nchini Afrika Kusini, ambayo ina moja ya viwango vya juu zaidi vya mauaji duniani.

Watu wengi wanamiliki bunduki zilizoidhinishwa kwa ulinzi wao binafsi, lakini kuna mzunguuko wa silaha nyingi zaidi zisizo halali.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW