Msemaji wa Kijeshi wa M23 auuwa DRC
1 Machi 2026
Matangazo
Tangazo hilo limejiri siku chache baada ya majeshi ya serikali ya Kongo kulenga kundi hilo karibu na mji wa Rubaya, eneo muhimu la uchimbaji madini katika wilaya ya Masisi, mkoa wa Kivu Kaskazini.
Katika taarifa yake M23 iliyosainiwa na msemaji wake wa kiraia, Lawrence Kanyuka imesema utawala wa Kinshasa umekiuka makusudi usitishaji mapigano na kutangaza vita kamili” kwa kuzindua mashambulizi ya droni nyuma ya mstari wa mbele wa vita.
Willy Ngoma na maafisa wengine watano wa makundi ya waasi mashariki mwa DRC waliwekewa vikwazo na Umoja wa Mataifa, wakituhumiwa kupanga au kutekeleza ukiukaji wa haki za binadamu na sheria ya kimataifa ya kibinadamu.