1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani: Kauli za Musk haziwezi kuisumbua Ujerumani

6 Januari 2025

Msemaji wa serikali ya Ujerumani amesema ushawishi wa bilionea wa teknolojia duniani Elon Musk kwa watu wa Ujerumani ni mdogo na hauna mashiko na kwamba machapisho yake hayawezi kuathiri nchi yenye watu milioni 84.

Kombo | Olaf Scholz und Elon Musk
Kansela Olaf Scholz Ujerumani na Mfanyabiashara wa Marekani Elon Musk Picha: Soeren Stache/dpa/picture alliance | Alain Jocard/AFP/Getty Images

Ujumbe huo wa msemaji wa serikali umetolewa siku chache baada ya Musk kumkosoa Kansela wa Ujerumani Olaf Schoz na kusema kwamba anakiunga mkono chama cha mrengo wa kulia kinachojiita mbadala kwa Ujerumani cha AFD kwenye uchaguzi ujao wa Ujerumani. Akigusia matamshi hayo, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema."Jambo muhimu ni kwamba Bwana Musk ameunga mkono upande wa chama chenye siasa kali za mrengo wa kulia na, kama unavyoona, hayafanyi hayo katika nchi hii tu. Jambo hilo  hatukubaliani nalo, na pia nalipinga." Viongozi wengine katika mataifa ya Ulaya ikiwemo Uingereza, Norway na Ufaransa wameonyesha kukerwa na kukemea kauli za bilionea huyo  katika mtandao wake wa X.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW