1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

MSF: Ugonjwa wa kipindupindu unaenea 'kwa kasi' Sudan Kusini

6 Desemba 2024

Wafanyikazi wa misaada nchini Sudan Kusini wametahadharisha juu ya mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu kaskazini mwa taifa hilo changa, ambako ghasia za muda mrefu zimelazimisha maelfu ya watu kuyahama makaazi yao.

MSF: Ugonjwa wa kipindupindu unaenea 'kwa kasi' Sudan Kusini
MSF: Ugonjwa wa kipindupindu unaenea 'kwa kasi' Sudan KusiniPicha: Fabio Bucciarelli/AFP via Getty Images

Shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka MSF limesema katika taarifa kuwa, wagonjwa 737 wa kipindupindu wameripotiwa katika jimbo la Upper Nile ndani ya muda wa mwezi mmoja.

Mlipuko wa ugonjwa huo umeripotiwa zaidi katika mji wa Malakal, lakini umeenea pia hadi maeneo mengine ya nchi ukiwemo mji mkuu wa Juba.

MSF yaeleza wasiwasi kuhusu hali nchini Sudan Kusini

Mji wa Malakal umepokea idadi kubwa ya raia wa Sudan Kusini waliorejea nchini humo kufuatia mgogoro katika nchi jirani ya Sudan, na umeorodesha wagonjwa 37,000 wa Kipindupindu kwa mujibu wa MSF.

Mkuu wa ujumbe wa shirika la madaktari wasiokuwa na mipaka MSF nchini Sudan Kusini Zakaria Mwatia amesema hali ni mbaya katika mji wa Malakal na kuna wasiwasi juu ya kuenea kwa ugonjwa wa kipindupindu katika maeneo jirani.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW