MigogoroHaiti
MSF yaimarisha uwepo wake nchini Haiti
6 Machi 2024Matangazo
MSF imesema kuwa idadi ya majeruhi wanaohitaji matibabu kutoka kwa makundi ya misaada ya shirika hilo imeongezeka kwa kasi.
Mkuu wa ujumbe huo wa MSF Mumuza Muhindo Musubaho, amesema vitanda vyote 50 katika hospitali yao ya Tabarre vina wagonjwa tangu mwanzoni mwa mwezi Februari, lakini mnamo Februari 28 hali ilizidi kuwa mbaya na kulazimika kuongeza idadi ya vitanda hivyo kufikia 75.
Soma pia: Watu kadhaa wauawa Haiti baada ya Gereza Kuu kuvamiwa
Musubaho ameongeza kuwa kwasasa, wanapokea idadi ya wastani ya majeruhi 5 hadi 10 kwa siku na kwamba wamefikia mwisho wa uwezo wao.
Huku hayo yakijiri, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kukutana katika kikao cha dharura baadaye leo kuhusiana na hali ya nchini Haiti.