MSF yalaani kuzuiwa kwa misaada ya kibinadamu Sudan Kusini
30 Januari 2026
Matangazo
Limesema hilo ndilo shirika la pekee la huduma za afya nchini humo linalowahudumia takriban watu 400,000, na kuongeza kuwa serikali imezuia safari za ndege za kibinadamu kwenda maeneo ya Lankien, Pieri, na Akobo, na kwamba pia imewazuia kusambaza madawa na wafanyakazi na kuwahamisha wagonjwa mahututi.
Katika taarifa yake, MSF imesema maafisa wa timu yake huko Pieri, walilazimika kuhama kituo chake jana kutokana na hatari ya kutokea kwa vita.
Pia waliwahamisha wagonjwa na kuchukuwa vifaa vya dharura walipokuwa wakiukimbia mji huo wakiwa na wakaazi wa eneo hilo.
Mkuu wa MSF tawi la Sudan Abdalla Hussein, amesema wagonjwa watakufa ikiwa serikali itaendelea kuzuia misaada ya kibinadamu na kupelekwa kwa huduma za matibabu Jonglei.