1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

MSF: Mzozo wa Sudan ni 'vita dhidi ya raia'

12 Oktoba 2024

Shirika la Madaktri wasio na mipaka MSF limeonya kuhusu kiwango cha njaa na utapiamlo katika maeneo makubwa ya taifa lililoharibiwa na vita la Sudan hasa katika mkoa wa Darfur.

Watoto wanakabiliwa na utapiamlo Sudan
Sudan inakabiliwa na vita iliyosababisha njaaPicha: Mohamed Zakaria//MSF/REUTERS

Uchunguzi uliofanywa kwa watoto 30,000 kwenye kambi ya wakimbizi ya Zamzam Kaskazini mwa  Darfur na Nyala kusini mwa jimbo hilo ulibainisha kuwa karibu theluthi ya watoto hao wana utapiamlo wa kiwango cha juu.

Soma zaidi: Kilicho nyuma ya vita ambacho kinasababisha njaa Sudan

Takwimu hizo zimetolewa na mratibu wa huduma za dharura wa shirika hilo, Claire Filippo katika ripoti aliyoitoa jijini Nairobi nchini Kenya. Sudan imekuwa ikikabiliwa na hali mbaya ya kiutu pamoja na njaa kutokana na vita vya kuwania madaraka vilivyoanza Aprili 2023 kati ya jeshi chini ya Jenerali Abdel Fattah al-Burhan dhidi ya kundi la RSF linaloongozwa na Mohammed Hamdan Daglo.