1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiJamhuri ya Kongo

MSF: Hali ya kutisha eneo la wakimbizi Shabindu-Kashaka

29 Novemba 2023

Shirika la Madktari Wasio na Mipaka MSF, limetahadharisha juu ya hali mbaya katika eneo la Shabidu-Kashaka linalowahifadhi wakimbizi waliotoroka vita na kundi la M23. MSF inasema hali ya kibinadamu huko inatisha.

Kongo DRC/MSF
MSF, yatahadharisha juu ya hali mbaya katika eneo la Shabidu-Kashaka, Nyiragongo mkoani Kivu Kaskazini Picha: DW/Flávio Forner

Tangu mapigano kati ya waasi wa M23 na vikosi vya jeshi la DRC kuanza upya huko Kitshanga, idadi kubwa ya watu wamehamia kwenye kambi za wakimbizi karibu na mji wa Goma. Wengi wao wamekimbilia katika eneo la wakimbizi la Shabindu-Kashaka.

Wimbi hili jipya la wakimbizi limekuwa likiishi kwa wiki mbili sasa katika hali ngumu sana, bila huduma za afya, bila vyoo, huku wakikabiliwa na hatari ya kupata magonjwa ya kuambukiza.

Dorcas Dada ni mkimbizi na mhudumu wa huduma ya kwanza. Anaelezea changamoto zinazohusiana na ukosefu wa vyoo kwa wakimbizi wapya, hali inayowafanya kwenda haja mahali popote.

Waasi wa M23 wachukua udhibiti wa mji wa kimkakati karibu na Goma

"Na kutokana na kukosekana kwa vifaa vya kazi, ninafunika kinyesi kwa majani ya mti, ambayo kwa bahati mbaya watu hawa wanayachukua tena kujilaza juu yake. Hii ni hatari sana na inaongeza hatari ya maambukizi. Kipindupindu kinaanza kuleta madhara hapa. Kama mwakilishi wa jamii, hii inanisumbua sana," alisema. 

Mmoja wa afisa wa shirika la Madktari Wasio na Mipaka MSFPicha: BARBARA DEBOUT/AFP

Hali mbaya imepelekea kutokea kwa vifo vya kwanza Jumatatu, Novemba 27. Wakimbizi waliokuwa na magonjwa sugu wanakabiliwa na ugumu wa kupata vituo vya afya. Hali hiyo ni sawa na wanawake wajawazito na watoto.

Sasa jamii ya kibinadamu inakabiliwa na dharura ya afya inayokua, kulingana na Baraka Kasau Binjamin, mmoja wa wanachama wa kamati ya uongozi wa kambi hii mpya ya wakimbizi.

M23 wakiteka tena kijiji cha Kishishe mashariki mwa Kongo

"Usimamizi wa kundi hili jipya la wakimbizi unaonekana kuwa mgumu kidogo. Tatizo kubwa ni suala la makazi na riziki. Ikiwa wahudumu wa kibinadamu wangewafikiria pia wakimbizi wa Shabindu, hii ingeweza pia kupunguza mateso ya waathirika wa vita hivi. Jana pekee tulirekodi kifo, mtu aliyekuja akiwa mgonjwa akafariki na kuzikwa moja kwa moja," alisema Binjamin. 

Madaktari wa MSF wapo kwenye eneo hilo ili kuwahudumia watu wanaohitaji matibabu kwa haraka. Lakini wahudumu hao wanashindwa kutoa huduma inavyopaswa kutokana na kuwepo idadi kubwa ya watu.

MSF yalemewa na idadi kubwa ya watu

Baadhi ya wakimbizi kutoka Congo, wakionekana katika kambi ya Rusayo nje kidogo ya mji wa Goma, inayotoa hifadhi kwa maelfu ya wakimbizi waliopoteza makaazi yao Mashariki kwa Congo kunakoshuhudiwa mapigano ya mara kwa maraPicha: Alexis Huguet/AFP

Shirika la madaktari wasio na mipaka limeitaka jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za haraka ili kuwezesha kupelekwa haraka vifaa vya matibabu muhimu, pamoja na aina nyingine za misaada ya kibinadamu inayohitajika ili kuwapunguzia mateso wakimbizi wa Shabindu-Kashaka.

Mkuu wa UNHCR ziarani Burundi kuwatembelea wahamiaji wa DRC

"Tumeanza miradi ya kutoa majibu, lakini kwa bahati mbaya, licha ya majibu haya, hatuwezi kuyafikia maeneo yote. Tunatoa tahadhari juu ya hali ambayo imekuwa ngumu kwa miezi kadhaa na inaweza kuwa mbaya zaidi na wimbi hili jipya la watu," alisema Jacob Grad-Jeux kutoka MSF.

"Kwa hiyo, tunachotaka, na tunachokiomba kwa ushirikiano wa kibinadamu na mamlaka washirika, ni kutoa majibu yanayofaa kwa mahitaji tunayokutana nayo kuhusu afya, lishe, makazi, na maji kwa watu waliokimbia," aliongeza.

Utata unaendelea kuwapo tangu kufikiwa suluhisho la amani la mzozo huu, hapo Machi 2022. Hali hiyo inaongeza wasiwasi na hatari kwa watu waliokimbia vita pamoja na jamii zinazowakaribisha, na kuzidisha wasiwasi unaokua kuhusu hali ya kibinadamu ambayo tayari ni ya.

UN: Watu 450,000 wameyakimbia mapigano mashariki mwa DRC

Wasiwasi huo ni pamoja na kitisho cha kupungua kwa rasilimali za jamii na ukosefu wa ufumbuzi wa matatizo ya binadamu yanayosababishwa na ukubwa wa mgogoro huo.

Pia ni muhimu kutambua kwamba idadi kubwa ya wanawake na watoto inaonyesha haja ya kuwepo na juhudi zitakazolenga kuyalinda makundi haya dhaifu zaidi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW