MSF yawataka wapiganaji Kongo kutozishambulia hospitali
9 Machi 2024MSF imesema kuwa wanaume waliokuwa wamejihami kwa silaha, walishambulia mji wa Drodro katika jimbo la Ituri usiku wa Machi 6 na 7 na kumuuwa mgonjwa mmoja mzee aliyekuwa amelala kitandani na pia kuiba vifaa vya matibabu.
Soma pia:Watu 15 wameuawa na maelfu wamekimbia mashambulizi ya waasi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Maelfu ya watu wametafuta hifadhi umbali wa kilomita 10 kutoka kambi ya watu wanaoishi na ulemavu ya Rho, iliyojengwa kutoa hifadhi kwa watu wasiozidi 30,000 lakini kwasasa ina watu mara mbili zaidi ya idadi hiyo.
Soma pia:Wakaazi mashariki mwa Congo wakabiliwa na uhaba wa chakula
MSF imewaondoa kwa muda wafanyakazi wake kutoka Drodro, na wakati ikiendelea kutoa huduma ya matibabu kwa watu hao katika kambi ya Rho, imesema hatua hiyo sio endelevu.
Meneja wa mpango wa MSF kwa Kongo Stephanie Giandonato, amesema kilichotokea katika eneo hilo ni jambo la kutia hofu.