1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MSF yawatibu wahanga wengi wa ubakaji Kongo

1 Oktoba 2024

Shirika la Madaktari Wasiokuwa na Mipaka (MSF) limesema limetibu idadi kubwa ya wahanga wa ubakaji mwaka jana katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kongo, ubakaji, dhuluma za kingono
Shirika la MSF limewatibu wanawake zaidi ya 25,000 wahanga wa dhuluma za kingono mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Picha: Habibou Bangre/AFP/Getty Images

Shirika hilo la msaada lilisema siku ya Jumatatu (Septemba 30) kwamba kwa kiasi kikubwa unyanyasaji huo umefanyika mashariki mwa Kongo ambako makundi ya wapiganaji yamedaiwa kufanya uhalifu huo.

Kwa mujibu wa shirika hilo, zaidi ya wahanga 25,000 wa vitendo vya ubakaji walihudumiwa mwaka 2023 na madaktari wasiokuwa na mipaka.

Soma zaidi: Wabakaji Bint wa Yombo wafungwa maisha, faini milioni moja

Ripoti ya shirika hilo imeongeza kusema kwamba idadi hiyo ya wahanga ndio kubwa zaidi kuwahi kurekodiwa nchini Kongo.

Wengi wa wahanga hao walitibiwa wakiwa kwenye makambi ya walioachwa bila makaazi karibu na mji wa Goma.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW