1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mshambuliaji timu ya taifa Gabon Aaron Boupendza amefariki

16 Aprili 2025

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Gabon Aaron Boupendza amefariki akiwa na umri wa miaka 28 baada ya kuanguka kutoka ghorofa ya 11 nchini China.

 

Shirikisho la soka la Gabon (FEGAFOOT) limetangaza kifo hicho leo Jumatano.

Kupitia taarifa kwenye mtandao wa X, shirikisho hilo la soka la Gabon limeandika kuwa Boupendza atakumbukwa kama mshambuliaji maahiri aliyeacha alama ya kudumu katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika yaliyoandaliwa nchini Cameroon mwaka 2022.

Marokko ikicheza na Gabon 2021(CAN)Picha: AFP via Getty Images

Boupendza, aliyejiunga na klabu ya Zhejianga FC ya China mapema mwaka huu, alikuwa katika fomu nzuri ya mchezo kwa kufunga mabao manne katika mechi sita.

Mamlaka nchini China zimeanzisha uchunguzi kubaini iwapo kuanguka kwake ilikuwa ni ajali, jaribio la kujiua au  tukio la uhalifu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW