Mshauri wa masuala ya usalama wa Marekani aitembelea China
27 Agosti 2024Mshauri wa masuala ya usalama wa taifa nchini Marekani,Jake Sullivan ameitembelea China, ni ziara yake ya kwanza nchini humo katika kipindi cha miaka minane. Sullivan amepokelewa katika uwanja wa ndege wa Beijing na wawakilisho wa wizara ya mambo ya nje ya China pamoja na balozi wa Marekani mjini Beijing Nicholas Burns. Mshauri huyo wa masuala ya usalama wa rais Joe Biden amepangiwa kuwa na mazungumzo na waziri wa mambo ya nje wa China Wang Ying katika ziara yake hiyo iliyopangwa kuendelea hadi Alhamisi.Xi: China na Marekani zapaswa kuwa washirika, sio washindani
China imesisitiza mara kadhaa juu ya umuhimu wa kufanyika mazungumzo kati ya mataifa hayo mawili yenye nguvu ambayo mahusiano yao yameharibika vibaya katika miaka ya hivi karibuni.China imesitisha mazungumzo ya kudhibiti silaha na Marekani
Miongoni mwa ajenda zinazotegemewa kujadiliwa ni migogoro ya Ukraine na Mashariki ya kati lakini pia mivutano iliyopo katika eneo la bahari ya Kusini mwa China na suala la Taiwan.