1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaVenezuela

Machado "Nalenga mabadiliko ya amani baada ya Maduro"

12 Desemba 2025

Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Maria Corina Machado amesema leo kwamba Rais wa Venezuela Nicolas Maduro ataondoka tu madarakani, ima kwa makubaliano ama la.

Norway Oslo 2025 | Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel María Corina Machado akiwasalimia watu kutoka kwenye Hoteli ya Grand
Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Maria Corina Machado akionyesha ishara ya kusalimia akiwa kwenye hoteli ya Grand baada ya binti yake Ana Corina Sosa Machado, kukubali tuzo hiyo kwa niaba yake, huko Oslo, Norway Desemba 11, 2025.Picha: Leonhard Foeger/REUTERS

Kiongozi huyo wa upinzani nchini Vanezuela aliwasili mjini Oslo mapema jana, akipuuzilia mbali zuio la muda mrefu la kusafiri alilowekea na mamlaka za Venezuela baada ya kujificha kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Machado alipozungumza na waandishi wa habari amesisitiza kwamba Maduro ataachia madaraka kwa makubaliano ama pasipo makubaliano, lakini akisema kwa sasa amejikita katika mabadilishano ya mpangilio na amani.

Machado alizuiwa kugombea katika uchaguzi wa rais mwaka jana, licha ya ushindi mkubwa alioupata kwenye uchaguzi wa awali wa upinzani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW