1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMali

Mshirika wa Waziri mkuu wa Mali Boubacar Traore akamatwa

29 Mei 2024

Mwanasiasa wa Mali Boubacar Traore amewekwa rumande na atafikishwa mahakamani mwezi Julai. Inajiri baada ya vuguvugu la M5-RFP kutoa taarifa kali dhidi ya makanali waliokamata madaraka katika mapinduzi ya mwaka wa 2020.

Mali | Choguel Kokalla Maiga
Vuguvugu la M5-RFP nchini Mali limegawanyika katika makundi mawili tofautiPicha: Nicolas Remene/MAXPPP/dpa/picture alliance

Maiga hajatoa kauli kuhusu kukamatwa huko na haijabainika kama aliiunga mkono taarifa hilo au la. Vuguvugu la M5-RFP limegawanyika katika makundi mawili tofauti. Maiga alikuwa ametangaza kuwa utawala wa kijeshi utaandaa tu uchaguzi mara baada ya hali ya usalama kutulia kabisa.

Soma pia: AU yairai Mali kuweka wazi mpango kuelekea demokrasia

Duru ya idara ya mahakama imesema Traore aliwekwa rumande kwa kuhujumu taifa, kuidharau mahakama, kuvuruga utulivu wa umma na kuchapisha taarifa za uwongo.

Kesi yake imepangiwa kuanza Julai mosi. Traore ni mshirika wa pili wa Maiga ambaye amewekwa jela baada ya Abdelkader Maiga kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jelakwa kosa la kumchafulia jina mnamo Aprili.