1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaRwanda

Mshukiwa wa mauaji ya kimbari ya Rwanda akamatwa Uholanzi

3 Oktoba 2023

Afisa wa zamani wa jeshi la Rwanda ambaye anashukiwa kuhusika katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda amekamatwa hii leo nchini Uholanzi.

Rückgabe sterblicher Überreste aus Deutscher Kolonialzeit
Picha: Vacca/Emblema/ROPI/picture alliance

Pierre-Claver Karangwa, mwenye umri wa miaka 67, amekamatwa kufuatia uchunguzi uliobaini jukumu lake katika mauaji hayo.

Waendesha mashtaka walianzisha uchunguzi huo baada ya Mahakama ya Juu ya Uholanzi kusema mwezi Juni mwaka huu kuwa Karangwa hawezi kurejeshwa Rwanda wakihofia kuwa asingelitendewa haki.

Karangwa anayeishi nchini Uholanzi tangu mwaka 1998, anashutumiwa na Rwanda kwa kuwa na jukumu kubwa katika mauaji ya Watutsi wapatao 30,000 katika parokia ya Mugina karibu na mji mkuu wa Rwanda, Kigali.

Takribani watu 800,000 wa kabila la Kitutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa mwaka 1994 nchini Rwanda wakati wa mauaji hayo ya kimbari.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW