1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mshukiwa wa ugaidi Ujerumani ajinyonga

Jane Nyingi
13 Oktoba 2016

Maafisa wanataka majibu baada mshukiwa wa ugaidi  kujiua gerezani. Jaber Albakr alipatikana akiwa amejinyonga  katika chumba cha  gereza alilokuwa akizuiliwa  katika mji wa Leipzig.

Polizei Sachsen Fahndungsbild Jaber Albakr
Picha: Polizei Sachsen

Waziri wa usalama wa ndani Thomas de Maziere amesema  kifo cha Albakr huenda kikavuruga  juhudi za kuwasaka washirika wake. Wakili wa Al Bakr Alexander Huebner mwanasheria wa mji wa  Dresden, ameliambia gazeti la Focus kuwa gereza la Leipzig lilikuwa linafahamu kuwa mteja wake  alikuwa katika hatari ya  kujiua baada ya kuonyesha dalili hizo.

Mkimbizi huyo kutoka Syria  alijiua jana usiku,siku mbili baada ya kutiwa mbaroni.Vyombo vya habari hapa ujerumani viliripoti kuwa mtuhumiwa huyo alifanikiwa kujinyonga  japo msemaji wa wizara ya sheria katika jimbo la Saxony Joerg Heroid  hakuthibitisha taarifa hiyo au kutoa maelezo zaidi.Mamlaka katika jimbo hilo ilikuwa tayari inakosolewa, baada ya mshukiwa huyo raia wa Syria  kufanikiwa  kuwakwepa polisi siku ya jumamosi walipokuwa wakijitayarisha  kuvamia ghorofa alilokuwa akiishi katika mji wa Chemnitz. Ndani ya chumba alichokuwa akiishi polisi walikuta bomu la uzito wa gramu 1.5  na alikuwa akitumia mtandao kupata maelekezo ya kutengengeza bomu hilo.

Jemgo alikokamatwa Jaber Albakr Picha: DW/N. Conrad

Jaber Albakr hakuonyesha dalili zozote za kuwa hatari

Albakr, ambaye alikuwa  amepewa hifadhi  baada ya kuingia Ujerumani mwaka uliopita hatimae alitiwa mbaroni jumatatu wiki hii  eneo la Leipiz baada ya raia wengine  wa Syria wanaoishi eneo hilo kumfunga kwa kamba na kisha  kuwaarifu polisi. Mshukiwa huyo  alipewa hifadhi  baada ya kuwasili nchini Ujerumani mwaka uliopita  na alikuwa  akifwatiliwa na wapepelezi  tangu mwezi uliopita.Hapo jana waziri wa uslama wa ndani De maziere  alisema raia huyo wa Syria  alikuwa ameshachunguzwa na kuthibitika kwamba hakuonyesha dalili zozote za kugeuka na kuwa hatari. Maofisa Ujerumani waasema inaaminika  mshukiwa huyo alikuwa  na  ushirikiano na kundi linalojiita dola la Kiislamu IS , na walidhani alikuwa anapanga kuushambulia uwanja wa ndege wa Berlin wiki hii.

Uwanja wa ndege wa Schönefeld BerlinPicha: picture-alliance/dpa/M. Gambarini

 

Raia watatu wa Syria waliomtia mbaroni Jaber Albakr w amepewa rasmi uhamisho na waziri de Maizere alisema wanahitaji pongezi na kutambuliwa kutokana na ujasiri wao.Polisi bado wanamzuiliwa mtuhumiwa mwingine anayeshukiwa kupanga shambulizi hilo la bomu lilotibuliwa ambae jina lake limetambulishwa tu kama Khalil A kuambatana na sheria za Ujerumani za kutofichua siri ya mtu binafsi. Mshukiwa huyo mwenye umri wa miaka 33 raia wa Syria  alikuwa akiishi  ghorofa la Chemnitz ambako polisi walikuta   bomu hilo .

Mwandishi:Jane Nyingi/AP/APE

Mhariri:Yusuf Saumu