1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Msiba wa kifo cha Kofi Atta Annan Mmagazetini

Oumilkheir Hamidou
20 Agosti 2018

Kifo cha katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan, mazungumzo kati ya kansela Angela Merkel na rais wa Urusi Vladimir Putin mjini Berlin na misaada kwa Uturuki ni miongoni mwa mada magazetini.

Kofi Annan und Angela Merkel
Picha: picture-alliance/Pressefoto Ulmer/B. Hake

 Tunaanza na msiba wa yule ambae gazeti la mjini Cologne, "Stadt Anzeiger" linamtaja kuwa "Mshika bendera miongoni mwa waadilifu duniani": Kofi  Atta Annan. Gazeti la "Nordwest-Zeitung" linahisi si jambo la kustaajabisha kwamba kifo cha katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan , Donald Trump , hakipi umuhimu mkubwa kuandika japo mstari mmoja katika mtandao wake wa Twitter. Gazeti linasema rais wa Marekani hajui aseme nini mbele ya kiongozi huyo anaeheshimika ulimwenguni na madilifu.

Tangu alipoanza kusumbuliwa na maradhi, msimu wa kiangazi mwaka huu  Annan alilalamika dhidi ya kupungua maadili Umoja wa Mataifa. Kwamba hali hiyo inafungamana moja kwa moja na jina la Trump, ameepuka kusema mwanadiplomasia mkuu huyo mstaafu. Licha ya utaratibu na ukakamavu , aliwajibika kwa dhati na kwa kila hali kwaajili ya Umoja wa Mataifa. Tabia yake ya upole itakumbukwa daima katika enzi hizi za makelele na watu kutunisha misuli."

Ziara ya  Vladimir Putin Berlin

Rais wa Urusi Vladimir Putin alikuwa ziarani mjini Berlin mwishoni mwa wiki. Mada ambazo huenda zilijadiliwa ni nyingi kuanzia mzozo wa Ukraine, kupitia Syria , mradi wa gesi ya Urusi na kadhalika. Hakuna lakini taarifa rasmi iliyochapishwa mwishoni mwa mazungumzo yao yaliyofanyika katika kasri la Meseberg, umbali wa kiomita 60 kaskazini mwa mji mkuu Berlin. Gazeti la "Badische Zeitung" linaandika: "Wajerumani wanastahiki kujua Putin anakusudia nini hasa anapoomba msaada wa mabilioni ya Euro kwaajili ya ujenzi mpya, vita vitakapomalizika kwa ushindi wa mshirika wake Assad. Ni sawa kwamba hakuna anaetaka kuiona Syria ikiendelea kusalia magofu. Hali ya utulivu nchini humo ambayo pia ni kwa masilahi ya Ulaya, haiwezi kupatikana bila ya msaada wa kimataifa.

Lakini mamilioni ya wasyria hawakukimbia mapigano tuu, wameukimbia pia utawala wa kiimla wa Assad.  Katika nchi wanakoandaamwa na kuteswa, hawatokubali kurejea. Assad anabidi ang'atuke ili kurahisisha suluhu ya kweli. Putin akifanikiwa kulifikia hilo hapo watu wanaweza kuzungumzia kuhusu misaada ya Umoja wa Ulaya."

 

Uhusiano wa Uturuki na Ulaya

Mada yetu ya mwisho magazetini inahusu misaada kwa Uturuki. Gazeti la "Badische Neusste Nachrichten" linaandika: "Kati ya Berlin na Ankara, mazungumzo yanabidi yaendelezwe sawa na uhusiano wa kiuchumi na yote mengine yanayobidi kuendelezwa. Kurejea uhusiano wa kirafiki kama zamani itawezekana tu ikiwa Erdogan ataanza upya kufuata njia ya demokrasia. Maafa ya Uturuki wa kulaumiwa si mwengine isipokuwa  yeye mwenyewe rais wa nchi hiyo.

 

Mwandishi:  Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW