Safari ya viongozi wa ulimwengu huanzia mbali sana. Katika #msichanajasiri wiki hii, tunamwangazia Zainab Masoud kiongozi wa wanafunzi wenye mahitaji maalum katika chuo Kikuu Cha Ustawi Wa Jamii, kilichoko Dar es salaam Tanzania.
Kipindi hiki kinakupa fursa ya kusikia ujasiri wa msichana na mchango mkubwa anaoufanya katika jamii. Msichana Jasiri ni muwazi, ana upendo na yuko tayari kujitoa kuwahudumia wengine. Ni shujaa!