1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Msikiti mwengine wachomwa moto Rotterdam

15 Juni 2005

Rotterdam:

Msikiti mmoja katika mji wa Uholanzi wa Rotterdam , umehujumiwa kwa moto , katika tukio linaloonekana kuwa la kibaguzi. Wengi wanaosali katika msikiti huo ni watu wa jamii ya Wasurinam. Polisi imesema umeharibiwa vibaya na kulikua na maadishi ya kibaguzi kutani. Kumekuweko na mlolongo wa vitendo vya kuitia moto misikiti nchini Uholanzi tangu mtengenezaji sinema aliyekua akiukosoa Uislamu Theo van Gogh alipochomwa kisu na kuuwawa mjini Amsterdam mwezi Novemba mwaka jana. Mholanzi mwenye asili ya Morocco ameshtakiwa kwa mauaji hayo. Jumatatu iliopita, Mholanzi mmoja alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela ambapo miezi sita kati ya hiyo ilifutwa, kwa kosa la kuanzisha moto kwenye msikiti mmoja mjini Rotterdam, akipinga mauaji ya van Gogh.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW