1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Msukosuko wa fedha

24 Februari 2009

Unaathiri baadhi ya viwanda vya Ujerumani.

Sio msukosuko wa hivi sasa tu wa kiuchumi ulimwenguni ambao unaviumiza kichwa viwanda vya asili na jadi vya Ujerumani kama vile Rosenthal,Schiesser au Marklin ambavyo mnamo karne iliopita vimekabiliana sawa sawa na misukosuko kadhaa.Katika kuporomoka chini kwa viwanda hivi vya zamani , sio kusema uongozi wake mara nyingi sio dhamana.

Saa za chapa Junghans zawakilisha mila na desturi za Schwarzwald.lakini kiwanda hicho cha kutengeza saa kilikawia mno kujirekebisha kwamba badala ya kuacha kuunda saa kwa wingi kubadili na kutengeneza saa kiasi lakini za hadhi ya juu.Matokeo yake, ni kupatwa na hasara kubwa ya mamilioni ya fedha.

Sasa makampuni mengi yanayotangaza kufilisika ni mkisa kimoja kimoja sio jumla jamala- anadai Prof.Frank Wallau kutoka Taasisi ya taftitishi za viwanda vya wastani mjini Bonn.

Anataja kwamba nchini Ujerumani kuna kuna makampuni na viwanda milioni 3.5 na 95% kati ya hivyo vimo mikononi mwa familia.

"Siwezi kudai makampuni yote yanafuata desturi za kizamani au zikihifadhi sana mikakati yao .Nixdorf kwa jicho langu, ni mfano halisi: Kampuni la Nixdorf mnamo miaka ya 1960/70 , ni la awali kabisa katika z sekta ya zana za komputa nchini Ujerumani.Kuingia kwa Bill Gate, ilikuja kutenganishwa Hard na sofware. Huu ni mfano usio mwema.Tunajionea mfano mwengine ambamo kampuni au kiwanda hakifuati kila mtindo mpya unaochomoza.Kwa mfano, kujitanua zaidi hadi nchini China na kutohamishia uzalishaji wa bidhaa sehemu nyengine na juu ya hivyo viwanda hivyo bado ni hayi na imara."Asema Prof.Wallau.

Viwanda na makampuni ya kale vinakabiliwa na changamoto za mashindano ya utandawaz.Kwa mfano kiwanda cha radio na TV cha GRUNDIG kilianza kuporomoka pale makampuni mengine ya TV ya kijapani yalipotia mguu wake barani Ulaya.Kiwanda cha zana za michezo PUMA kiliweza tu kubaki hayi katika kiwanda cha ukoo cha Gucci na Tchibo na hata wao wamehusika na kuharakisha biashara ulimwenguni.

Kwa muujibu wa Profesa Wallau,viwanda na makampuni ya kijerumani, ni miongoni mwa wale walioneemeka mno na mfumo wa utandawazi-globalisation.

Prof.Wallau anatarajia kwahivyo,mwaka huu , viwanda vingi vitatangaza kufilisika.Mwaka 2008 idadi ya makampuni yaliofilisika ilipungua, lakini tangu mwishoni mwa mwaka jana pale msukosuko wa fedha Ujerumani ulipochukua mateka wake wa kwanza, viwanda vingi vilianza kupata hasara kubwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW