1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mtaalamu wa teknolojia ya habari akutwa na hatia ya uhaini

29 Oktoba 2024

Mtaalamu wa teknolojia ya habari, Firuz Dadoboyeb, amehumikiwa adhabu ya kifungo cha miaka 13 na nusu jela nchini Urusi kwa madai ya kujaribu kutoa siri za serikali kwa shirika la ujasusi la Marekani, CIA.

USA | CIA
Nembo ya shirika la ujasusi la Marekani, CIA.Picha: Dennis Brack/Danita Delimont/imago images

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali, mahakama ya mjini Moscow ilimtia hatiani mtaalamu huyo kwa kosa la kutenda uhaini kwa manufaa ya Marekani.

Shirika la habari la serikali nchini Urusi TASS, limeripoti taarifa hiyo kwa kulinukuu shirika la usalama la Urusi, FSB. 

Shirika hilo la usalama limesema mtaalamu huyo alijipatia habari kinyume cha sheria ambazo zilikuwa siri ya serikali na alikuwa anapanga kuzipeleka kwa jasusi mmoja wa Marekani.

Firuz Dadoboyev alikamatwa mnamo mwaka 2022 na tangu wakati huo amekuwa akisisitiza kuwa ametubu vitendo vyake.